• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapata mkopo wa dola milioni 25 za kimarekani kwa ajili ya miradi ya maji

    (GMT+08:00) 2018-06-14 10:02:40

    Waziri wa maji na umwagiliaji wa Tanzania Bw Isaac Kamwelwe amesema kwamba serikali ya Tanzania imepata mkopo wa dola milioni 25 za kimarekani kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya miradi ya maji iliyoko mjini Dar es Salaam.

    Akiongea bungeni mjini Dodoma Bw. Kamwelwe amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kutatua changamoto za maji zinazowakabili watu zaidi ya milioni 5 walioko mji wa Dar es Salaam, ambazo zitaondolewa wakati miradi hiyo ya maji itakapozinduliwa. Ameongeza kuwa miradi hiyo itaanzishwa katika mwaka wa fedha ujao.

    Ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia imeonyesha kuwa ukosefu wa maji nchini Tanzania umekuwa kikwazo kwa ukuaji wa uchumi na upunguzaji wa umaskini nchini humo. Tanzania inahitaji kurekebisha usimamizi wa maji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako