• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SADC yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uelewa juu ya Ualbino

    (GMT+08:00) 2018-06-14 10:25:03

    Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imetoa wito wa kupinga kwa pamoja aina zote za dhuluma, chuki na ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wa Ualbino.

    Katibu mtendaji wa SADC Bibi Stergomena Lawrence Tax amesema katika taarifa kwamba katika sehemu nyingi duniani, ikiwa ni pamoja na nchi za kusini mwa Afrika, ualbino unaeleweka vibaya na albino wanaendelea kuishi na hofu, kutokana na mashambulizi, mauaji na ubaguzi wa kijamii dhidi yao. Amezipongeza nchi wanachama wa SADC ambazo zimeweka sera ya kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi katika sheria.

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kutokomeza ubaguzi dhidi ya ualbino, na kusema kuwa mengi zaidi yanaweza kufanywa ili kuongeza uelewa wa umma juu ya ulemavu huo wa ngozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako