• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wiki ya Biashara ya China yaanza Kenya

    (GMT+08:00) 2018-06-14 10:37:08

    Awamu ya nne ya Wiki ya Biashara ya China imeanza mjini Nairobi, na wateja wa ndani wameeleza shauku yao kwa bidhaa zinazotengenezwa China.

    Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushirikiano wa Kenya Bw. Adan Mohamed ameungana na maofisa kutoka makampuni makubwa ya China kuzindua maonyesho hayo ya biashara ya siku tatu. Amesema China bado ni mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara kwa Kenya, na Kenya inalenga kuongeza biashara ya bidhaa na huduma kati ya nchi hizo mbili.

    Wiki ya Biashara ya China ya mwaka 2018 imevutia makampuni 500 ambayo yameonyesha bidhaa zao za kielektroniki, vifaa vya umeme, simu za mkononi, nguo, vifaa vya ujenzi, chakula na vinywaji.

    Bw Mohamed pia amesema Kenya itahimiza uhusiano wa kibiashara na China ili kutimiza Ajenda yake ya Big Four ya kuhimiza uzalishaji viwandani, usalama wa chakula, upatikanaji wa nyumba za bei nafuu na huduma za matibabu kwa wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako