• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yavitaja migogoro na uchumi mbaya chanzo cha watu wengi wa Sudan Kusini kutokuwa na nchi

    (GMT+08:00) 2018-06-14 10:37:39

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema kukimbia makazi kutokana na mapigano na taabu za kiuchumi kumesababisha baadhi ya watu wa Sudan Kusini kutokuwa na nchi wakati wanakataliwa au kushindwa kumudu kupata nyaraka za uraia.

    UNHCR imesema changamoto kuu kwa wakimbizi wa ndani kupata nyaraka za utaifa ni kuwa wanahitaji mashahidi.

    Kwa mujibu wa Idara ya Uraia, Pasipoti na Utambuzi ya Sudan Kusini, waombaji wa wanaotiliwa shaka wanatakiwa kupata nyaraka za mapendekezo kutoka mamlaka za maeneo wanayoishi, kitu ambacho ni kigumu kwa wakimbizi wa ndani.

    Ripoti iliyotolewa na UNHCR imesema ni vigumu kwa wakimbizi wa ndani kupata nyaraka za uraia kutokana na unyonge mkubwa wa kiuchumi, unaowafanya washindwe kumudu ada ya dola za kimarekani 25 hadi 37.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako