• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yazindua mpango mpya wa kuongeza tija ya udongo Afrika

    (GMT+08:00) 2018-06-14 10:38:04

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO kwa kushirikiana na Shirika la Udongo Duniani limezindua mpango mpya wa kusaidia kuongeza tija ya udongo kwa asilimia 30 katika nchi 47 za Afrika.

    Mashirika hayo yamesema mpango huo uitwao "Afrisoils" pia unalenga kupunguza kwa asilimia 25 hali ya kuvia kwa udongo katika miaka kumi ijayo barani Afrika, ambako ni chini ya nusu ya ardhi inayofaa kwa kilimo, na asilimia 16 tu ndio ina rutuba.

    Mkurugenzi mkuu msaidizi wa FAO anayeshughulikia hali ya hewa, viumbe anuwai, ardhi na maji Bw. Rene Castro, amesema ni usimamizi wa kudumu wa udongo ndio unaoweza kuhakikisha maendeleo kwenye sekta ya kilimo, usalama wa chakula na kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako