• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa China katika nchi za nje waongezeka kwa kasi katika miezi mitano iliyopita

    (GMT+08:00) 2018-06-14 17:15:18

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng leo kwenye mkutano na waandishi wa habari ametoa takwimu mbalimbali za uchumi na biashara, akisema katika miezi mitano iliyopita uwekezaji wa China katika nchi za nje umefikia dola za kimarekani bilioni 47.89, ambalo ni ongezeko la karibu asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, wakati huo huo China imevutia uwekezaji wa nchi za nje wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 52.66, ambalo ni ongezeko la asilimia 1.3.

    Bw. Gao Feng amesema, katika miezi mitano iliyopita mwaka huu, uwekezaji wa China katika nchi za nje umeendelea kwa utulivu, wakati huo huo muundo wa uwekezaji huo umeboreshwa kwa mfululizo tangu China iongeze nguvu ya kuchunguza uwekezaji usiofaa. Anasema, "Katika miezi mitano iliyopita, uwekezaji wa China katika nchi za nje haswa umeingia katika sekta za huduma, uzalishaji, madini na mauzo ya jumla na rejareja. Hakuna mradi mpya katika sekta za ujenzi wa nyumba, michezo na burudani."

    Sehemu za mashariki zimeendelea kuongoza uwekezaji katika nchi za nje, huku mashirika ya mikoa mitatu ya kaskazini mashariki yakiongeza uwekezaji kwa kiasi kikubwa. Takwimu zinaonesha kuwa katika miezi mitano iliyopita, mikoa hiyo mitatu iliwekeza dola za kimarekani bilioni 1.43 katika nchi za nje, ambalo ni ongezeko la asilimia 88.2 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

    Takwimu za wizara ya biashara pia zinaonesha kuwa, katika miezi mitano iliyopita, matumizi ya uwekezaji wa nchi za nje nchini China yameongezeka kwa kiasi kidogo. Bw. Gao Feng ameeleza sekta za uzalishaji wa teknolojia ya juu imevutia uwekezaji mwingi zaidi kutoka nje. Anasema,

    "Sekta za uzalishaji wa teknolojia ya juu imevutia uwekezaji kutoka nchi za nje wenye thamani ya dola za kimarekani zaidi ya bilioni 52.6, ambalo ni ongezeko la asilimia 61.9%."

    Takwimu zinaonesha kuwa uwekezaji kutoka nchi za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki na nchi za Ukanda Mmoja na Njia moja umeongezeka kwa asilimia karibu 40, na uwekezaji kutoka Singapore, Korea ya Kusini, Japan, Marekani, Uingereza na Macao pia umeongezeka kidhahiri.

    Licha ya hayo, takwimu zilizotolewa na forodha zinaonesha kuwa katika miezi mitano iliyopita, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje imefikia dola za kimarekani trilioni 1.8, na ongezeko la oda za China kwa bidhaa kutoka nchi za nje limeendelea kuzidi ongezeko la mauzo ya bidhaa za China katika nchi za nje. Bw. Gao Feng anasema,

    "Katika siku zijazo, China itazingatia zaidi sifa na ufanisi wa mauzo ya bidhaa katika nchi za nje badala ya kasi ya ongezeko. Katika soko la kimataifa, tutahimiza uwezo mpya wa ushindani kama vile teknolojia, chapa na huduma bora."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako