• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani atarajia Korea Kaskazini kuchukua hatua kubwa katika kupunguza silaha za nyuklia

    (GMT+08:00) 2018-06-14 18:47:42

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema, anatarajia Korea Kaskazini itapata maendeleo makubwa katika kupunguza silaha za nyuklia ndani ya miaka miwili na nusu ijayo.

    Bw. Pompeo ambaye yuko ziarani nchini Korea Kusini, amesema, rais Donald Trump wa Marekani ameeleza wazi kuwa, ahadi yake ya kusimamisha mazoezi ya kijeshi na Korea Kusini itatekelezwa kama mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini yataendelea vizuri.

    Bw. Pompeo pia amesema, makubaliano yaliyofikiwa na Marekani na Korea Kaskazini hayakuonekana kwa kikamilifu kwenye taarifa ya pamoja, ikimaanisha kuwa juhudi nyingine nyingi zinahitajika kufanyika katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako