• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kitabu kuhusu mawazo ya Xi kuhusu uandishi wa habari chachapishwa

    (GMT+08:00) 2018-06-14 18:52:52

    Kitabu kuhusu fikira za Xi Jingping kuhusu uandishi wa habari kimechapishwa na Idara ya Uchapishaji ya Umma na Kampui ya Uchapishaji ya Xuexi.

    Kitabu hicho, ambacho kimeandaliwa na Idara ya Habari ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kinapatikana katika matawi ya duka la vitabu la Xinhua nchi nzima.

    Kuanzia mkutano mkuu wa 18 wa CPC, Xi, ambaye ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, ametoa mfululizo wa maoni mapya, hatua na mahitaji ya kuimarisha na kuboresha kazi za umma za Chama, na ametoa majibu ya masuala mfululizo ya kimsingi, kimkakati, na ya jumla yanayohusiana na maendeleo ya muda mrefu ya kutangaza kazi za Chama kwa umma.

    Kitabu hicho kinatoa ufafanuzi wa kina na mrefu kuhusu mawazo ya uandishi ya Xi na kina maelekezo ya ngazi ya juu kwa waandishi wa habari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako