• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani

    (GMT+08:00) 2018-06-15 07:54:22

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo ambaye yuko ziarani hapa Beijing.

    Katika mazungumzo yao rais Xi amesema China na Marekani zinabeba majukumu muhimu katika kulinda amani na utulivu wa dunia, na kuhimiza maendeleo na ustawi wa dunia.

    Amesema anatumai kuwa pande hizo mbili zitafuata makubaliano yaliyofikiwa kati yake na rais Donald Trump kuhusu kuimarisha mawasiliano, kuongeza hali ya kuaminiana, kudhibiti mikwaruzano, kupanua ushirikiano, na kuendeleza uhusiano kati ya pande hizo mbili kwenye njia sahihi, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili na dunia nzima.

    Bw. Pompeo amefikisha shukurani za rais Donald Trump kwa rais Xi, hususan kutokana na msaada muhimu aliotoa rais Xi katika suala la nyuklia la Peninsula ya Korea. Bw. Pompeo amesema Marekani inapongeza mchango wa China katika kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kwa njia ya kisiasa, pia inapenda kushirikiana na China katika kuondoa silaha za nyuklia katika Peninsula hiyo, na kuleta amani ya kudumu kwenye kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako