• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 13 wafariki ajali ya basi magharibi mwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-06-15 09:05:56

    Polisi nchini Tanzania wamesema watu 13 wamefariki dunia na wengine 50 wamejeruhiwa baada ya basi waliokuwa wanasafiria kupinduka mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa Tanzania. Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Bw. Mussa Taibu amesema ajali hiyo ilitokea jana saa tisa aslasiri kwenye eneo la Igodima, na basi hilo lililokuwa na abiria 63 lilikuwa likielekea Mbeya kutoka Tabora. Dereva na askari 12 wa jeshi la Tanzania ni miongoni mwa waliofariki kwenye ajali hiyo. Bw. Taibu amesema kuendesha kwa uzembe ni moja ya vyanzo vya ajali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako