• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapanga bajeti ya uchumi wa viwanda kwa mwaka mpya wa fedha

    (GMT+08:00) 2018-06-15 09:47:14

    Serikali ya Tanzania imetangaza maeneo manne ya vipaumbele na miradi ya maendeleo kwa mwaka mpya wa fedha, ikiweka mkazo kwenye ujenzi wa viwanda na kuhimiza ongezeko la uchumi.

    Akiwasilisha ripoti ya uchunguzi kuhusu hali ya uchumi kwa mwaka jana, ni mipango ya maendeleo kwa mwaka mpya wa fedha, Waziri wa Fedha na mipango wa Tanzania Dk Philip Mpango amesema mipango ya maendeleo italenga kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara na kuendeleza raslimali watu.

    Bw. Mpango amesema asilimia 37 ya bajeti ya serikali kwa mwaka mpya wa fedha zimetengwa kwa ajili ya kazi hizo. Amesema lengo kuu la serikali ni kujenga viwanda vitakavyotumia bidhaa za ndani za kilimo kama malighafi, pamoja na madini na gesi asilia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako