• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yatoa wito wa kuongeza uwekezaji dhidi ya ukosefu wa damu

    (GMT+08:00) 2018-06-15 10:04:04

    Serikali ya Sudan Kusini imeadimisha Siku ya kuchangia damu duniani ikitoa wito wa kuongeza uwekezaji kwenye sekta ya huduma za utoaji damu nchini humo.

    Waziri wa afya wa Sudan Kusini Bw Riek Gai Kok amesema Sudan Kusini imekumbwa na hali mbaya ya miundombinu ya afya, inayokwamisha huduma za utoaji damu nchini kote, lakini juhudi zimefanywa kwa ajili ya kuboresha hali hiyo.

    Amesema kwa sasa kuna benki moja tu ya damu nchini Sudan Kusini, hali ambayo imesababisha vifo vya watu wengi kutokana na ukosefu wa damu. Ametoa wito kwa wenzi wa maendeleo watoe misaada ili kuhimiza huduma za utoaji damu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako