• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 53 wafariki dunia kutokana na kimbunga cha kitropiki Somalia

    (GMT+08:00) 2018-06-15 10:04:24

    Shirika la kuratibu misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) limesema watu wasiopungua 53 wamefariki dunia na wengine takriban laki 2.29 wameathiriwa kutokana na kimbunga cha kitropiki kiitwacho Sagar, ambacho kilisababisha mvua kubwa na mafuriko huko Somaliland na Puntland, kaskazini mwa Somalia mwezi uliopita.

    OCHA imenukuu habari kutoka idara za usimamizi wa maafa za Somalia kuwa watu 50 wamefariki huko Somaliland na wengine watatu wamekufa katika eneo la Puntland.

    Ofisa wa OCHA amesema mvua kubwa na mafuriko yameleta hasara kubwa kwa miundombinu na mashamba, na kusababisha vifo vya watu wengi na kuwafanya wengine wakose makazi. Miundombinu ya kimsingi ikiwemo maji na vifaa vya mawasiliano imeharibiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako