• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaharakisha kujenga mfumo wa muamana

  (GMT+08:00) 2018-06-15 17:32:47

  China inaharakisha kujenga mfumo wa muamana. Ofisa wa idara kuu ya maendeleo na mageuzi ya China leo hapa Beijing amesema, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei, mahakama zimetangaza orodha ya watu milioni 10.89 waliofanya makosa ya muamana, na kati yao milioni 2.54 walitekeleza wajibu wao ili kuepuka kuadhibiwa. Baadaye China itaendelea kusukuma mbele ujenzi wa mfumo wa jumla wa muamana, kwa kuharakisha kujenga mfumo mpya wa usimamizi, kuimarisha ujenzi wa mfumo wa muamana katika sekta muhimu, na kukamilisha utaratibu wa kutuza na kutoa adhabu.

  Naibu mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa sera ya idara kuu ya maendeleo na mageuzi ya China ambaye pia ni msemaji wa ofisi hiyo Bibi Meng Wei, leo amesema, hivi karibuni tovuti ya "Muamana ya China" imeonesha orodha ya kikundi cha kwanza cha watu 169 watakaowekewa kizuizi cha kusafiri kwa ndege na treni, kwa kufanya makosa mabaya ya muamana, yakiwemo kukataa kulipa ushuru, udanganyifu wa hisa, na kufanya makosa waliposafiri kwa ndege na treni.

  Bibi Meng amesema makosa ya muamana ya kuadhibiwa yataendelea kuongezeka. Kwa mujibu wa waraka wa kumbukumbu wa kuadhibu makosa ya muamana katika sekta ya utalii uliotolewa hivi karibuni, mashirika na maeneo ya utalii, pamoja na watu wanaoshughulikia utalii wakifanya makosa ya muamana, watakabiliwa kwa vifungu 36 vya adhabu. Wakati huo huo ufanisi wa adhabu hizo umeonekana. Bibi Meng anasema,

  "Hadi kufikia mwishoni mwa Mei, mahakama zimetangaza orodha ya watu milioni 10.89 waliofanya makosa ya muamana, ambao waliadhibiwa na idara husika, kwa vile kupigwa marufuku kusafiri kwa ndege na treni. Watu hao ni pamoja na wakuu laki 2.65 wa mashirika."

  Wakati huo huo, utaratibu wa kutuza watu wenye muamana pia umeanzishwa kwa pande zote. Bibi Meng amesema, China imeanza kutekeleza mradi wa "Muamana +", anasema,

  "Madhumuni ya kuanza kwa mradi huo ni kuwawezesha watu wenye muamana mzuri kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi. Huduma hizo haswa ni kupata idhini za serikali, kukopa fedha benki, kukodi vifaa na vyumba vya ofisi, na kusafari kwa ndege na treni. Katika siku zijazo, huduma hizo zitaongezeka zaidi, ili kuwahamasisha watu wawe na muamana."

  Kuhusu hatua muhimu zijazo, Bibi Meng amesema China itaharakisha kujenga utaratibu mpya wa usimamizi, kuimarisha ujenzi wa muamana katika sekta muhimu, kukamilisha mfumo wa jumla ya kutuza na kutoa adhabu kwa sheria zinazohusika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako