• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mshauri wa ngazi ya juu wa China atembelea eneo la kibiashara liliwekezwa na China nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2018-06-15 19:01:24

    Mshauri wa kisiasa wa ngazi ya juu wa China Wang Yang ametembelea eneo la kibiashara lililowekezwa na China lililoko mjini Kapeeka, wilaya ya Nakaseke, mkoa wa Kati nchini Uganda, na kuzitaka kampuni zaidi za China kuendeleza biashara zao barani Afrika.

    Wang, ambaye ni mwenyekiti wa kamati kuu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, ametembelea eneo hilo katika ziara yake ya siku nne nchini Uganda. Akiwa kwenye eneo hilo, Wang alitembelea viwanda vinavyofanya uzalishaji, kuongea na wafanyakazi kutoka Uganda na China, na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa kampuni zilizowekeza hapo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako