• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijana wa Uganda ashinda zawadi kwa kuvumbua kifaa cha kupima malaria bila kutumia damu

    (GMT+08:00) 2018-06-16 16:24:10

    Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 24, aitwaye Brian Gitta, raia wa Uganda ameshinda zawadi ya mvumbuzi bora inayotolewa kila mwaka na Chuo cha taaluma ya Uhandisi cha nchini Uingereza, baada ya kuvumbua kifaa kwa ajili ya kupima na kutambua ugonjwa wa malaria bila ya kutumia damu ya mgonjwa kama ilivyo desturi ya maabara.

    Gitta pamoja na wenzake, wametengeza kifaa kidogo ambacho hakiihitaji utaalam katika kukitumia ambapo chenyewe humhitaji mgonjwa kukiweka kwenye kidole chake na kwa namna kilivyotengenezwa hutambua mabadiliko ya maumbo, rangi pamoja na wingi wa chembe hai nyekundu za damu ambazo zimeathirika kwa malaria.

    Kwa ushindi huo, Gitta amezawadiwa fedha taslimu pauni za Uingereza 25,000 sawa na dola za kimarekani 33,197 kwa uvumbuzi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako