• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China ina imani ya kupata ushindi kwenye mapambano dhidi ya kujilinda kibiashara kwa Marekani

  (GMT+08:00) 2018-06-16 19:24:14

  Tarehe 15 mwezi Juni serikali ya Marekani ilitangaza orodha ya bidhaa za China zitakazoongezwa asilimia 25 ya ushuru wa forodha, ambazo inahusisha bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 zinazoagizwa kutoka China kwa mwaka. Hatua hii imekiuka na kuharibu sana maslahi halali ya China na wananchi wake. Halafu serikali ya China ilitoa taarifa ikitangaza kuongeza asilimia 25 ya ushuru wa forodha kwa bidhaa za aina 659 za Marekani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50.

  Hatua ya China imeonyesha imani yake ya kulinda maslahi ya kitaifa na maslahi ya wananchi, na kulinda utandawazi wa dunia na mfumo wa biashara unaoshirikisha pande nyingi.

  Bidhaa za aina 369 zilizotangazwa na China ni pamoja na mazao ya kilimo, magari, bidhaa za kemikali, vifaa vya matibabu na bidhaa za nishati.

  Hatua ya China si kama tu inaonyesha msimamo wa serikali ya China, bali pia inaonyesha nguvu, kasi, na imani za wachina wote, ambazo kiuhalisia ni silaha yenye nguvu kubwa kwa China kupata ushindi kwenye vita ya biashara.

  Ukweli wa historia umethibitisha kuwa, hakuna mshindi kwenye vita ya biashara. Lakini Marekani iliharibu ahadi zake mara kwa mara, na kufanya vita ya biashara, kitendo hicho cha Marekani si kama tu kimepunguza uaminifu wake mbele ya wananchi wa China na Marekani, bali pia kitazifanya nchi zinazofanya mazungumzo ya kibiashara na Marekani zipoteze imani nayo . Shirikisho la biashara la Marekani, shirikisho la wauzaji rejareja la Marekani, na shirikisho la soya la Marekani yalitoa taarifa kwa nyakati tofauti yakiilaani serikali ya Marekani, yakisema hatua ya serikali ya Trump ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China kwa kweli ni kutoza ushuru kwa wateja wa Marekani.

  Ikiwa nchi inayopenda amani na ushirikiano, China haipendi kufanya vita ya biashara, lakini China haiogopi kufanya vita ya biashara, kwani kitendo cha Marekani kimeharibu mazingira ya biashara ya kawaida ya China na mfumo wa kimataifa wa biashara unaoshirikisha pande nyingi. Ili kulinda maslahi ya muda mrefu ya wananchi na utaratibu wa biashara wa kawaida duniani, China imelazimika kujibu vita ya biashara.

  Kukabiliwa na vita ya biashara iliyofanywa na Marekani, China iko tayari. Vilevile China ina imani ya kupata ushindi, kwani China inaelewa kuwa, kwenye mapambano hayo ya muda mrefu yaliyo na utatanishi, China inaungwa mkono na watu wengi duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako