• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Ethiopia kufanya ziara ya kutuliza mzozo mkubwa katika jimbo la kusini

    (GMT+08:00) 2018-06-16 19:34:04

    Shirika la habari la Ethiopia EBC limetangaza kuwa waziri mkuu wan chi hiyo Abiy Ahmed anatarajiwa kutembelea mji wa Hawassa ambao umekuwa na vurugu zilizotokana na tofauti zilizojitokeza baina ya makabila mawili maarufu ya jimbo la kusini mwa Ethiopia.

    Waziri mkuu Ahmed anatarajiwa kufanya mkutano wa mazungumzo na wazee wa jamii hizo, pamoja na viongozi wa kiserikali wa eneo hilo ili kurejesha amani iliyotoweka.

    Katika mji wa Hawassa kwa muda mrefu kumeshuhudiwa vurugu zilizopelekea vifo vingi na watu wengine kulazimika kuyahama makazi yao kutokana na tofauti za muda mrefu ya haki ya umiliki na matumizi ya ardhi kati ya watu wa kabila la Sidamas na watu wa kabila la Wolaita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako