• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa UN asifu hatua ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-06-17 16:57:34

    Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Bw. Antonio Guterres ameunga mkono tangazo lililotolewa na serikali ya Afghanistan la kuongeza muda wa kusimamisha mapigano dhidi ya waasi wa Taliban.

    Katika taarifa aliyotoa kupita msemaji Stephane Dujarric, bwana Guterres pia amewataka Taliban kufuata wito wa watu wa Afghanistan wa kuhimiza amani na kuutekeleza kwa vitendo.

    Aidha, Bw. Guterres anaamini kuwa suluhu ya mgogoro wa Afghanistan itapatikana kupitia mchakato wa kitaifa nchini humo kati ya pande zinazohasimiana na kuonya wale wote wanaharibu mchakato wa kupatikana amani.

    Katika hatua nyingine Katibu wa Un amelaani shambulio lililotekelezwa siku ya jumamosi na kuua takribani watu 26 lililokuwa limelenga watu waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya Eidel Fitr katika jimbo la Kusini mwa Afghanistan la Nangarhar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako