• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la ndege la Ethiopia lapanga kuongeza maradufu ndege zake ndani ya miaka saba

    (GMT+08:00) 2018-06-18 08:20:07

    Shirika la ndege la Ethiopia ET limetangaza mpango wa kuongeza maradufu ndege zake hadi kufikia 200 ndani ya miaka saba. Ofisa mkuu wa biashara wa shirika hilo Bw.. Busera Awol amesema hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kudumisha hadhi yake ya uongozi barani Afrika, na mapema mwezi huu, shirika hilo lilisherehekea kukabidhiwa ndege yake ya 100, na linatarajia kuongeza ndege 19 zaidi katika miezi kumi ijayo. Imefahamika kuwa shirika la ndege la Ethiopia hivi sasa limekuwa na safari 112 za kwenda sehemu mbalimbali duniani, na lilikuwa ni shirika la kwanza la ndege la Afrika na la nne duniani kuanzisha safari za kuja China kuanzia mwaka 1973.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako