• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yatoa mafunzo kwa wahandisi 20 wa Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-06-18 08:50:57

    Kampuni ya uhandisi wa ujenzi wa reli ya China imetoa mafunzo bila malipo kwa wahandisi vijana 20 wa Sudan Kusini.

    Vijana hao wanaotoka kwenye maeneo ya ujenzi, ufundi umeme na useremala, walimaliza hivi karibuni mafunzo ya mwezi mmoja kwenye mradi unaofadhiliwa na China wa upanuzi wa hospitali ya mafunzo ya Juba, ambayo ni hospitali kubwa zaidi ya umma nchini Sudan Kusini.

    Kwa mujibu wa kampuni hiyo, vijana 7 kati ya hao 20 wamehitimu mafunzo hayo, nao wataajiriwa na kampuni hiyo.

    Mhandisi wa umeme Bw. Deng Agany Aguto aliyehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Rwanda, alisema kwenye mafunzo hayo amejifunza kufuata nidhamu, kuwa mvumilivu na kuchapa kazi, ambayo ni maadili muhimu kwa wahandisi.

    Mwakilishi wa Shirikisho la urafiki kati ya China na Sudan Kusini, Bw Dut Abednego, amesema pendekezo la kutoa mafunzo hayo lilitolewa mwezi uliopita, ambayo yanalenga kutoa ujuzi wa kiufundi kwa wanafunzi wa uhandisi na kuimarisha uhusiano katika wahandisi wa Sudan Kusini na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako