• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Kenya na Zambia wataka kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kiusalama kati ya nchi zao

    (GMT+08:00) 2018-06-18 09:06:13

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Edgar Lungu wa Zambia wamesema nchi zao zitahimiza ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama kati yao.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Nairobi baada ya mazungumzo kati yao, inasema viongozi hao wamekubaliana kuwa nchi zao zitahimiza ushirikiano kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na utalii, usafiri, biashara, uwekezaji na usalama wa kikanda. Sehemu ya makubaliano hayo ni pamoja na kuwapokea wanafunzi 50 kutoka Zambia kwenye chuo cha Utalii cha Kenya.

    Kenya na Zambia zimekuwa na uhusiano mzuri kwenye sekta ya kilimo, utalii, elimu na Tehama. Ikulu ya Kenya imesema nchi hizo mbili kwa sasa zimekuwa na makubaliano ya ushirikiano kwenye maeneo ya sayansi, teknolojia na uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako