• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Israel aonya kupambana na vikosi vya Iran kote nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-06-18 09:52:17

    Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya kuwa jeshi la Israel litachukua hatua dhidi ya vikosi vya Iran kote nchini Syria.

    Akihutubia mkutano wa baraza la mawaziri wa kila wiki, Bw. Netanyahu amesema Iran inapaswa kuondoa jeshi lake kutoka Syria. Pia amesema, hivi karibuni, amebadilishana maoni na rais wa Russia Vladmir Putin na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kuhusu hali ya kikanda na suala la Syria.

    Habari zinasema, Israel inaendelea kulaani Iran kupanua shughuli zake katika kanda ya Mashariki ya Kati, na kusisitiza kuwa haitaruhusu Iran kuifanya Syria kuwa mstari wake wa mbele wa kupambana na Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako