• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watatu wafariki katika tetemeko la ardhi nchini Japan

    (GMT+08:00) 2018-06-18 17:11:31

    Idara ya Hali ya Hewa ya Japan imesema, watu watatu wamefariki na wengine 51 kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.1 katika kipimo cha Richter lililotokea mkoani Osaka, Japan, leo asubuhi.

    Serikali imeanzisha kituo cha usimamizi wa dharura katika makazi ya waziri mkuu Bw. Shinzo Abe, ambaye amesema serikali itazingatia kanuni ya msingi ya kutoa kipaumbele kwa maisha katika kukabiliana na janga hilo na kujaribu kuwaokoa watu walioathirika.

    Idara ya Hali ya Hewa ya Japani imetoa wito kwa Wajapani kuangalia usalama wao binafsi na kuendelea kuwa makini kutokana na uwezekano wa kutokea matetemeko kama hayo wiki ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako