• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miradi ya upandaji miti yaboresha mazingira ya Tibet

    (GMT+08:00) 2018-06-18 17:14:10

    Mamlaka ya wilaya ya Ali katika mkoa unaojiendesha wa Tibet nchini China imesema itawekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 11 katika mradi wa upandaji miti kwa mwaka huu.

    Mamlaka ya misitu ya wilaya hiyo imesema, mradi huo unalenga kupanda miti kwenye heka 2,267 katika wilaya hiyo ambayo ina mazingira magumu, ambapo wakazi wa huko wamekuwa wakisumbuliwa na mchanga, upepo na ukame.

    Miradi ya upandaji miti ilizinduliwa kwenye miaka ya 1970 na 80, na mazingira yameboreka katika miaka ya karibuni kutokana na kuongezeka kwa fedha na hatua sahihi zilizochukuliwa ikiwemo kutambulisha miti inayovumilia baridi na ukame.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako