• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wa sehemu mbalimbali washerehekea Sikukuu ya Duan Wu

    (GMT+08:00) 2018-06-18 18:53:14

    Leo tarehe 5 ya mwezi wa tano kwa Kalenda ya kilimo ya China ni sikukuu ya Duan Wu nchini China, ambapo watu wa sehemu mbalimbali wanasherehekea sikukuu hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kufanya mashindano ya mbio za mashua ya Dragoni, kutengeneza chakula cha Zongzi, kutalii kwa magari ya n.k.

    Sikukuu ya Duan Wu ina historia ya zaidi ya miaka elfu mbili, na ilikuwa sikukuu muhimu kwa watu walioishi kwenye sehemu ya pwani ya kusini mashariki nchini China wakati wa kuabudu mungu wa maji au dragoni. Mshairi aliyeitwa Qu Yuan alijitupa mtoni baada ya taifa lake kushambuliwa na maadui katika siku hiyo, na baadhi ya sehemu zinamkumbuka mshairi huyo wakati wa siku hiyo. Sikukuu ya Duan Wu pamoja na sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina, siku ya Qing Ming pamoja na siku ya Mbalamwezi ni sikukuu muhimu nne za jadi za kichina. Mwaka 2009 sikukuu ya Duan Wu ilithibitishwa na kuorodheshwa kuwa urithi wa utamaduni usio wa mali duniani.

    Kati ya shughuli mbalimbali, mashindano ya mashua za dragoni ni shughuli muhimu ya kusherehekea sikukuu hiyo. Kwenye Bustani ya Ziwa la Qin mjini Taizhou, mkoani Jiangsu, watalii wengi wakiwa wamevalia nguo ya maalumk wanasubiri kupanda mashua za dragoni:

    "Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki katika mashindano haya ya mashua ya dragoni, lengo langu si kupata nafasi ya kwanza, bali ni kujiburudisha kwa kushiriki kwenye mashindano wakati wa Duan Wu."

    Siku tatu za mapumziko wakati wa sikukuu ya Duan Wu zimetoa fursa kwa wachina wengi kusherehekea sikukuu na familia yao, naibu katibu mkuu wa Taasisi ya mila na desturi za China Bibi Zhang Bo anaona kuwa, kadiri jamii inavyopata maendeleo, ndivyo sikukuu hii ya kijadi imeonegzwt mambo mengi mapya na kuiunganisha vizuri na maisha ya watu. Anasema:

    "Katika vipindi tofauti vya historia, njia za watu wa kusherehekea sikukuu za jadi zinabadilikabadilika. Tunatakiwa kujua chanzo na thamani ya sikukuu za jadi, na njia ya kusherehekea sikukuu za jadi zinaonesha utambuzi na maoni yetu kwa dunia tunayoishi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako