• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CEO wa Audi akamatwa na polisi kwa "kashfa ya dizeli"

    (GMT+08:00) 2018-06-19 08:51:50

    Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya magari ya Audi Bw. Rupert Stadler amewekwa kizuizini na polisi wa Ujerumani, wakati mamlaka za Ujerumani zinachunguza kashfa ya udanganyifu kuhusu kiwango cha utoaji wa moshi wa magari ya dizeli wanayotengeneza. Ofisi ya mwendesha mashtaka inayowajibika na uchunguzi huo inasema kukamatwa kwake kunatokana na uwekezano wa mtuhumiwa huyo kula njama na wahusika wengine. Taarifa iliyotolewa na kampuni mama ya Audi, Volksawgen imesema haitatoa maoni yoyote kuhusu kesi hiyo, lakini imesisitiza kuwa Bw. Stadler hana hatia hadi itakapothibitishwa kuwa ana hatia. Imefahamika kuwa wachunguzi wanaamini kuwa Audi imeuza magari laki 2.1 yaliyowekwa software ya udanganyifu kuhusu utoaji wa moshi kwenye masoko ya Marekani na Ulaya tangu mwaka 2009.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako