• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Ethiopia asema mapatano yanaleta mazingira mazuri ya usalama

    (GMT+08:00) 2018-06-19 09:06:49

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw Abiy Ahmed amesema juhudi za hivi karibuni zilizofanywa na serikali yake kuleta mapatano, zimeweka mazingira mazuri ya usalama na kuhimiza umoja miongoni mwa Waethiopia.

    Akiongea kwenye bunge la Ethiopia, Bw. Ahmed amesema juhudi mbalimbali za mapatano na mazungumzo yaliyofanywa na makundi mbalimbali zimeleta mazingira mazuri ya usalama.

    Bw. Ahmed aliingia madarakani mwezi Aprili mwaka huu, huku nchi yake ikiwa inakumbwa na maandamano ya kuipinga serikali ya mara kwa mara, hasa kwenye jimbo kubwa zaidi ya Ethiopia la Oromia, ambako ana uungaji mkono mkubwa.

    Hata hivyo wakati Bw. Ahmed akisema hayo wiki iliyopita vurugu ziliukumba mji mkuu wa jimbo la kusini, Hawassa, na kusababisha vifo vya watu 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako