• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kimataifa kuhusu ulinzi wa amani barani Afrika wafunguliwa Morocco

    (GMT+08:00) 2018-06-19 09:07:08

    Mkutano wa siku mbili wa kimataifa kuhusu changamoto za ulinzi wa amani barani Afrika umefunguliwa mjini Rabat, Morocco.

    Mkutano huo ulioandaliwa na jumuiya ya washauri bingwa ya Morocco, unawakutanisha mamia ya washiriki, ikiwa ni pamoja na maofisa waandamizi wa jeshi, wataalamu wa sheria, wahadhiri wa vyuo vikuu.

    Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Morocco Bw Youssef Amrani, amesema changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika ambazo ni pamoja na migogoro, ugaidi, uhamiaji na mabadiliko ya hali ya hewa, zinatakiwa kutatuliwa kwa kina.

    Ajenda za mkutano huo zinalenga mambo ya kisiasa na kimkakati kwenye ulinzi wa amani, mafanikio ya walinzi wa amani wa umoja wa mataifa, ulinzi wa raia, kujenga uwezo walinzi wa amani na operesheni za umoja wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako