• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika Kusini yafanya juhudi kufanikisha afya kwa wote

    (GMT+08:00) 2018-06-19 09:07:32

    Afrika Kusini inaendelea kupata mafanikio kwenye kutoa huduma za afya kwa nchi nzima.

    Naibu mkurugenzi wa Idara ya afya ya taifa Bw. Anban Pillay amesema hazina ya Afrika Kusini itakuwa na fedha za kuhakikisha watu wanapata huduma bora za afya kwa usawa kwenye hospitali binafsi na za umma. Pia amesema wanataka kuondoa kasoro ya watu kutotibiwa kwa wakati, na kutakuwa na utaratibu wa kitaifa wa kutoa dawa na kuzisambaza kwenye vituo vya afya.

    Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Bw. Aaron Motsoaedi anatarajiwa kuongea na vyombo vya habari kuhusu mswada wa bima ya afya ya taifa hivi karibuni, huku kukiwa na mwito wa kufanya huduma za afya ziwe sawa kwa maeneo ya mijini na vijijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako