• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Russia na Marekani wajadili mpango wa mawasiliano ya kisiasa kati yao

    (GMT+08:00) 2018-06-19 09:31:05

    Wizara ya mambo ya nje ya Russia imesema waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov na mwenzake wa Marekani Mike Pompeo wamejadili mpango wa mawasiliano ya kisiasa kati ya nchi hizo mbili katika siku za baadaye.

    Wizara hiyo pia imesema katika mazungumzo ya simu kati yao, pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni kuhusu azimio namba 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalohusu suala la Syria na kutoa mchango katika kutatua suala la peninsula ya Korea.

    Habari zinasema rais Donald Trump wa Marekani amesema, anaweza kukutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin katika majira ya joto ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako