• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa pande mbili za Sudan Kusini kukutana Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-06-19 09:31:26

    Kundi kuu la upinzani la Sudan Kusini SPLM/A-IO limethibitisha kuwa, kiongozi wake Bw.Riek Machar ameachiwa huru kutoka kwenye kizuizi cha nyumbani nchini Afrika Kusini na atakwenda Ethiopia kufanya mazungumzo na rais Salva Kiir.

    Hata hivyo serikali ya Sudan Kusini bado haijathibitisha kama Rais Kiir atafanya mazungumzo na Bw. Machar, licha ya kuwa hapo awali alikubali kukutana na Bw. Machar. Mkurugenzi wa habari na uhusiano wa umma wa SPLM-IO Bw. Puok Both Baluang amesema, Bw. Machar atakwenda Addis Ababa kushiriki kwenye mazungumzo hayo.

    Habari zinasema, viongozi hao wawili wamealikwa kwa waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed ili kuongeza jitihada za IGAD kusaidia kutatua mgogoro wa Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako