• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi kutoka nchi za Afrika Mashariki, Marekani na Umoja wa Ulaya vyafanya luteka ya pamoja nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2018-06-19 09:41:06

    Vikosi kutoka nchi za Afrika Mashariki, Marekani na Umoja wa Ulaya jana vimeanza luteka ya pamoja ya wiki mbili mashariki mwa Uganda.

    Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Richard Karemire amesema luteka hiyo ya pamoja ni kwa ajili ya kuongeza uwezo wao katika kukabiliana na matishio ya usalama ya kikanda na kuimarisha uwezo kwenye operesheni za kulinda amani.

    Kamanda wa jeshi la ardhini na vikosi vya ulinzi vya Uganda Meja Jenerali Peter Elwelu amefungua luteka hiyo mjini Jinja, mashariki mwa Uganda, ambayo imevivutia vikosi kutoka Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda, Somalia, Uholanzi na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako