• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yaanza kazi ya uhakiki wa idadi ya polisi wake

    (GMT+08:00) 2018-06-19 09:54:00

    Polisi nchini Uganda wameanza kazi ya kuhakiki idadi ya maofisa wake ili kutambua idadi ya polisi hewa.

    Naibu msemaji wa polisi Bw. Patrick Onyango amesema zoezi hilo lililoanza mjini Kampala pia litafanywa katika sehemu nyingine za Uganda ili kuhakiki polisi watoro na polisi hewa. Ameongeza kuwa timu ya ukaguzi wa mahesabu itapewa orodha ya malipo ya mishahara na kuikagua kulingana na ripoti za makao makuu ya jeshi la polisi.

    Zoezi hilo limefanywa kwa kufuata agizo la Inspekta jenerali wa polisi Martin Okoth Ochola aliyechukua nafasi hiyo kutoka kwa aliyekuwa mkuu wa polisi Jenerali Kale Kayihura.

    Imeripotiwa kuwa kuna maofisa wasiotekeleza majukumu, na wengine wamelikimbia jeshi, lakini bado wanaendelea kupokea mshahara kila mwezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako