• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM apinga kuwatenga watoto na wazazi wao wahamiaji

    (GMT+08:00) 2018-06-19 09:54:43

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema watoto hawatakiwi kudhuriwa kisaikolojia kutokana na kutengwa na wazazi wao, na umoja wa familia unapaswa kudumishwa.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Msemaji wake Bw. Stephane Dujarric, Bw. Guterres amesema ikiwa ni suala la kanuni, wakimbizi na wahamiaji wanapaswa kutendewa kwa heshima kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

    Zaidi ya watoto elfu 2 wameripotiwa kutenganishwa na wazazi wao walioingia Marekani kutoka Mexico kinyume cha sheria.

    Sera ya kupambana na uhamiaji haramu iliyotolewa hivi karibuni na serikali ya Marekani inayoongozwa na rais Donald Trump imekosolewa vikali ndani na nje ya nchi hiyo.

    Hata hivyo msemaji huyo amekana kuwa taarifa hiyo inatolewa dhidi ya sera ya Marekani, licha ya kukiri kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ana wasiwasi na hali kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani.

    Kwa mujibu wa kura za maoni za Chuo Kikuu cha Quinnipiac, asilimia 66 ya Wamarekani wanapinga sera yenye utata ya serikali ya rais Trump inayowatenga watoto na wazazi wao waliogunduliwa kuingia nchini humo kinyume cha sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako