Wizara ya Biashara ya China imesema hatua inayochukuliwa na Marekani ya kuishinikiza na kuisaliti China, inaenda kinyume na makubaliano yaliyofikiwa kwenye mazungumzo mengi kati ya nchi hizo mbili, na pia imeisikitisha jumuiya ya kimataifa. Marekani kuanzisha vita ya kibiashara hakulingani na kanuni za soko wala mkondo wa maendeleo ya dunia wa sasa, pia kumeharibu maslahi ya watu na makampuni ya nchi hizo mbili, na wa dunia nzima.
Wizara hiyo imeongeza kuwa China itachukua hatua zinazolingana na kitendo hicho cha Marekani, hii sio tu ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa na wananchi wa China, bali pia ni kulinda mfumo wa biashara huria na maslahi ya pamoja na binadamu. Bila kujali jinsi mazingira ya nje yanavyobadilika, China itafuata mpango wake, kutoa kipaumbele maslahi ya wananchi, kusukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango, kuhimiza ukuaji mzuri wa uchumi na kuongeza kasi ya kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |