• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taarifa ya Ikulu ya Marekani yasababisha malalamiko kutoka sekta mbalimbali nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-06-19 18:23:50

    Wadau wa sekta ya biashara, vyombo vya habari, na mashirikisho mbalimbali yamelalamikia taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani jana usiku kuwa itaandaa orodha ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 zitakazotozwa ushuru.

    Naibu mkurugenzi wa shirikisho la wakulima wa soya la Marekani Bw. David Stevens amesema, China ni nchi muhimu kwa kuwa ni soko kubwa zaidi linaloagiza soya, na Marekani haiwezi kustahamili kupoteza soko hilo.

    Naye Mkurugenzi wa Shirikisho la wauzaji wa rejareja la Marekani Bw. Matthew Shai amesema, vita ya biashara itaathiri vibaya uchumi wa Marekani na familia za kawaida za Wamarekani , pia itawafanya watu wengi kupoteza kazi zao. Amelitaka bunge la Marekani lichukue hatua na kuvunja hali ya kukwamwa ya sasa.

    Shirika la Habari la Marekani CNN limesema, kujilinda kibiashara kunatishia biashara duniani, pia kutaharibu uchumi wa Marekani na nafasi za ajira nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako