• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Gazeti la China lasema rais wa Marekani anacheza kamari kwa kutumia maslahi ya wamarekani

  (GMT+08:00) 2018-06-19 18:56:18

  Gazeti la Global Times la China limetoa makala likisema rais Donald Trump wa Marekani anacheza kamari na China kwa kutumia maslahi ya wamarekani. Hii ni kufuatia taarifa aliyoitoa jana kupitia Ikulu ya Marekani akiiagiza Ofisi ya wajumbe wa biashara ya Marekani, kuangalia uwezekano wa kuongeza ushuru wa forodha kwa asilimia 10 kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200.

  Rais Trump pia ametishia kuwa, endapo hatua ya China ya kulipiza kisasi kutoza ushuru wa forodha bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 zitatekelezwa, mpango huo wa Marekani wa kuongeza utozaji wa forodha pia utatekelezwa. Na kama China itachukua hatua mpya za kulipiza kisasi, Marekani pia itajibu kwa kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200.

  Makala ya Gazeti la Global Times imeeleza kuwa, China haitaki vita vya kibiashara na Marekani, na hadi sasa bado haijatangaza hatua yoyote ya kukabiliana na hatua za Marekani, na hatua ya China ya kutoza ushuru wa forodha inalenga kujibu hatua ya Marekani kutoza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China ambayo ilikiuka kanuni za WTO.

  Makala hiyo inasema, taarifa hiyo ya rais Trump imeonesha kwamba anataka vita vya kibiashara na China, akiitaka China kuvumilia ili kudhibiti maeneo ya vita vya kibiashara, na kupora mali za China kwa kukiuka kanuni ya biashara ya kimataifa, na kuwafurahisha wananchi wake. Ukweli wa mambo ni kuwa, rais Trump anazingatia kura wakati wa uchaguzi mkuu tu.

  Lakini kitendo hicho cha rais Trump ni kama kucheza kamari. Makala hiyo imesema inasikitisha kama rais Trump anaona kuwa anaweza kupata ushindi, na China itavumilia tu kukabiliwa na mpango wa Marekani wa utozaji wa ushuru wa forodha. Je, licha ya China, nchi nyingine zilizotozwa ushuru wa forodha na Marekani zikiwemo nchi za Ulaya, Canada na Mexico, ni nchi gani imevumilia?

  Kitendo hicho cha serikali ya rais Trump si kama tu kimeathiri maslahi ya wachina, bali pia ameweka maslahi ya wamarekani hatarini: Upatikanaji wa nafasi za ajira nchini Marekani utaathirika na bei za bidhaa pia zitapanda. Ustawi wa Marekani unategemea sana uhusiano kati yake na mtandao wa uchumi duniani, je, kama utaratibu wa uchumi wa kimataifa utavurugika, Marekani itawezaje kupata faida peke yake tu?

  Makala hiyo pia imeeleza kuwa, Marekani siku zote inafanya mahesabu yenye makosa kwa biashara kati yake na China, ikitangaza kuwa urari wa biashara kati ya China na Marekani umezidi dola za kimarekani bilioni 370, lakini kiasi hicho hakihusishi thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 ya biashara ya mauzo ya nje ya Marekani kwa kupitia upande wa tatu, na utoaji wake wa huduma kwa China. Lakini serikali ya Marekani haiwezi kuidanganya China, badala yake imejidanganya ikiamini kuwa kama vita vya kibiashara ikitokea, China itaishiwa hatua za kuchukua. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa, ikiwa Ikulu ya Marekani itazusha vita, kamwe China haitaishiwa hatua za kuchukua.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako