• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yazindua mitaala mipya ili kuboresha upatikanaji wa elimu

    (GMT+08:00) 2018-06-19 19:42:43

    Somalia imezindua mitaala mipya ya elimu ya shule za msingi nchini humo ili kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kwa vijana wa nchi hiyo.

    Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu, Utamaduni na Elimu ya Juu nchini humo Hassan Mohamed Ali. Amesema mtaala huo mpya utaanza kutekelezwa kwenye mwaka mpya wa masomo unaoanza Agosti, na anatumai kuwa mtaala huo mpya utatoa mchango mzuri kwa elimu ya watoto wa Somalia.

    Mtaala huo mpya wa masomo ulitangazwa jana wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika zilizofanyika mjini Mogadishu, ambapo serikali iliahidi kufanya kazi kwa karibu na wenzi wa maendeleo ili kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kwa vijana wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako