• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yakanusha kupanga kuongeza ukomo wa masafa ya makombora

    (GMT+08:00) 2018-06-20 08:32:02

    Jeshi la Iran limesema Iran haihitaji kuongeza ukomo wa masafa ya makombora yake zaidi ya kilomita elfu mbili za sasa. Kamanda mkuu wa jeshi la Iran Bw. Mohammad Ali Jafari, amesema wana uwezo wa kuongeza ukomo wa masafa ya makombora, lakini sera yao ni kudumisha masafa ya kilomita elfu mbili, kwa kuwa inatosha kufikia shabaha zote za kimkakati. Bw. Jafari pia amelaani anachokiita "tishio la Marekani la kudhoofisha uwezo wa ulinzi na makombora wa Iran". Mwezi Mei rais Donald Trump alitangaza kuitoa Marekani kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran, na kusema makubaliano hayo hayawezi kuleta amani katika eneo la Mashariki ya Kati, kwa kuwa hayahusishi mpango wa Iran wa kuendeleza makombora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako