• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapongeza ushirikiano na China katika kuhifadhi utamaduni na urithi wa asili

    (GMT+08:00) 2018-06-20 08:45:52

    Serikali ya Kenya imepongeza ushirikiano uliopo kati ya China na Kenya kwenye kuhimiza uhifadhi wa utamaduni na urithi wa asili. Katibu mkuu tawala wa Wizara ya michezo na urithi ya Kenya Bw Hassan Noor Hassan, amesema Kenya iko tayari kunufaika na ushirikiano kati yake na China kwenye uhifadhi wa utamaduni na uwepo wa viumbe anuai.

    Bw. Hassan amesema wanasayansi wa Kenya wanapokea uungaji mkono kutoka kwa China kupitia mafunzo yanayowawezesha wanasayansi wa Kenya kupata udhamini wa masomo ya shahada ya uzamivu ya uhifadhi wa viumbe anuai, kwenye vyuo vikuu vya China.

    Mbali na udhamini huo, Kenya pia imenufaika kwa msaada uliotolewa na kampuni ya Tencent ya China kuzindua maktaba ya kidigitali, na kuweka michezo ya jadi ya Kenya kwenye mfumo wa kidigitali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako