• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yasema nchi za Afrika kaskazini zapata mafanikio zaidi kuelekea malengo ya maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2018-06-20 09:16:12

    Ripoti iliyotolewa jana na taasisi ya malengo ya maendeleo endelevu ya Afrika (SDGC/A) imeonesha kuwa nchi za Afrika kaskazini zimepata mafanikio makubwa zaidi kuelekea malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

    Ripoti hiyo iliyotolewa kutokana takwimu za mashirika ya kimataifa kama yale ya Umoja wa Mataifa, benki ya maendeleo ya Afrika na makala za kitaaluma, imesema kanda ya Afrika Kaskazini imechukua nafasi ya kwanza kuelekea kutimiza malengo hayo, wakati nchi za Afrika ya kati na mashariki zimechukua nafasi za mwisho.

    Ripoti pia imesema, ingawa nchi za Afrika zimefanya vizuri katika kutimiza malengo 13 ya masuala ya hali ya hewa, bado zina pengo kubwa la kutimiza malengo yanayohusu miundombinu, afya, haki, kilimo, usalama wa chakula na nishati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako