• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar yakamata chakula kilichopita muda kilichoagizwa kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani

    (GMT+08:00) 2018-06-20 09:16:34

    Serikali ya Zanzibar imetangaza kukamata tani 140 za chakula kilichopita muda wake, kilichoagizwa kwa ajili ya matumizi ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

    Mkurugenzi mtendaji wa Wakala wa chakula na dawa Zanzibar (ZFDA) Bw. Burhan Simai, amesema chakula hicho kilichoagizwa kwa ajili ya matumizi kwenye mfungo wa Ramadhani na sikukuu ya Idi, ni pamoja na tani 40 za mchele, tani 75 za unga wa sembe, tani 25 za sukari na lita elfu 15 wa mafuta ya kupikia.

    Habari zinasema shirika hilo pia limekamata dawa na vipodozi, ikiwa ni pamoja na chanjo 4,000 za ATS, vilivyoagizwa kutoka nchi za Asia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako