• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dunia yatakiwa kuisaidia Afrika kuzoea mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-06-20 09:26:55

    Mkutano wa 5 wa kimataifa kuhusu kuzoea mabadiliko ya hali ya hewa umefunguliwa jana mjini Cape Town, Afrika Kusini, ambapo wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wametoa mwito kwa dunia kuisaidia Afrika kuzoea mabadiliko ya hali ya hewa.

    Mkutano huo wa siku tatu umefanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika, na kutilia mkazo udhaifu wa nchi za Afrika katika mabadiliko ya hali ya hewa. Wajumbe wamekubaliana kuwa athari ya kuongezeka kwa joto barani Afrika ni kubwa ikilinganishwa na hali ya hewa ya kihistoria ambayo mfumo wa binadamu na wa asili umebadilika.

    Ripoti iliyotolewa kwenye mkutano huo imeonyesha kuwa, matukio mabaya ya hali ya hewa kama vile ukame, mafuriko na joto kali yanatokea mara kwa mara barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako