• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Kenya zakubaliana kuimarisha uhusiano

    (GMT+08:00) 2018-06-20 09:27:34

    Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Wang Yang amemaliza ziara yake nchini Kenya, ambako alikutana na rais Uhuru Kenyatta, spika wa baraza la chini la bunge la Kenya Bw Kenneth Lusaka, na spika wa baraza la Seneti Bw. Justin Muturi.

    Bw. Wang Yang amepongeza maendeleo makubwa ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kusema, ushirikiano kati ya China na Kenya umekuwa mfano mzuri wa ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesema mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi Septemba mjini Beijing, utatangaza hatua mpya za ushirikiano kati ya China na Afrika, ambazo zitahimiza China na Afrika kutimiza maendeleo ya pamoja na ya kunufaishana kwenye kiwango cha juu zaidi.

    Rais Kenyatta amesema Kenya inaunga mkono China kuandaa mkutano wa FOCAC, na inapenda kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili na kuunganisha vizuri mkakati wa maendeleo ya kila upande. Ameikaribisha China kupanua uwekezaji nchini Kenya, na kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako