• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yaihimiza Afrika kuanzisha ushirikiano wa sekta binafsi na umma ili kutatua upungufu wa fedha

    (GMT+08:00) 2018-06-20 09:50:17

    Benki ya Dunia imezihimiza serikali za Afrika kuanzisha ushirikiano wa sekta binafsi na umma (PPP) ili kutatua upungufu wa fedha kwenye sekta ya miundo mbinu.

    Kiongozi wa mradi wa ongezeko lenye usawa, fedha na taasisi katika Benki ya Dunia Bw. Johan Mistiaen, amesema mjini Nairobi kuwa upungufu wa fedha kwenye sekta ya miundo mbinu barani Afrika ni mkubwa, na hauwezi kutatuliwa kwa raslimali za umma au mashirika ya maendeleo ya kimataifa peke yake.

    Kwenye uzinduzi wa tovuti ya mradi wa ushirikiano wa sekta binafsi na umma nchini Kenya, Bw. Mistiaen amesema Benki ya Dunia inazihimiza serikali za Afrika kuimarisha mipango ya ushirikiano huo ili kushirikisha sekta binafsi katika kuendeleza miundombinu muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako