• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yajitoa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-06-20 10:11:40

    Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Bibi Nikki Haley ametangaza kuwa Marekani itajitoa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

    Hii ni mara nyingine kwa Marekani kujitoa kwenye mashirika na mikataba ya kimataifa, baada ya kujitoa kwenye Makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, Mkataba wa Umoja wa mataifa kuhusu uhamiaji, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, na makubaliano ya nyuklia ya Iran.

    Katika mkutano na wanahabari pamoja na waziri wa mambo ya nje Bw. Mike Pompeo, Bibi Haley amesema Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeshindwa kutekeleza "mageuzi makubwa na ya kimfumo" kama ilivyoagiza Marekani hapo awali, kwa hivyo Marekani imeamua kujitoa rasmi kutoka baraza hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako