• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano ili kuendeleza soka: Ligi Kuu za Tanzania na Hispania zaingia mkataba

    (GMT+08:00) 2018-06-20 10:13:52

    SHIRIKISHO la Soka nchini Tanzania (TFF), jana limetangaza kuwa limeingia mkataba wa miaka mitatu na Ligi kuu ya nchini Hipania (LA LIGA) kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu nchini Tanzania.

    Lengo kuu la mkataba huo, ni kushirikiana katika Nyanja mbalimbali za kisoka kupitia michakato tofauti, ikiwemo semina na mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika kuendeleza soka, uongozi wa soka na waamuzi.

    Waliohudhuria utiaji saini huo uliofanyika nchini Hispania, ni Rais wa TFF Walles Karia na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura, kwa upande wa La Liga walikuwa Rais wa La Liga Javier Tebas, Mkurugenzi wa Maendeleo ya kimataifa wa La Liga Oscar Mayo, na mwakilishi wa Laliga nchini Tanzania Sami Hanane.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako