• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tennis: Maendeleo ya Rwanda katika mashindano ya dunia kanda ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-06-20 10:14:29

    Timu ya taifa ya vijana ya Rwanda imeanza vibaya mashindano ya dunia ya mchezo wa tennis yanayoendelea nchini Kenya, baada ya kufungwa na Nigeria kwa alama za jumla 3-0.

    Rwanda ilishindwa katika mechi 3, moja ikiwa ni kati ya Ernest Habiyambere aliyefungwa na Emmanuel Sylvester kwa seti ya 6-1 na 7-5, lakini pia Joseph Ubon wa Nigeria alimshinda Olivier Haguvimana kwa seti ya 6-0 na 6-1.

    Na kwa upande wa wachezaji wawili wawili pia Nigeria iliifunga Rwanda, na katika mashindano hayo katika kanda ya Afrika, Rwanda iko kundi A pamoja na timu za Benin, na Cameroun.

    Katika mechi nyingine zilizopigwa jana, wenyeji Kenya wameendeleza wimbi la ushindi kwa kuwafunga Msumbiji kwa alama 3-0 za jumla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako