• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tennis: Murray asema ushiriki wake kwenye michuano ya Wimbledon utaamuliwa na maendeleo ya Afya yake

    (GMT+08:00) 2018-06-20 10:14:45

    Mchezaji wa kimataifa wa Tennis kutoka Scotland Andy Murray amesema maendeleo yatakayopatikana katika afya yake, hasa wiki ijayo baada ya mashindano ya Eastbourne nchini Uingereza ndiyo yataamua iwapo atashiriki michuano ya Wimbledon mwezi ujao au la.

    Murray ameyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza baada ya kutocheza kwa mwaka mmoja kutokana na majeruhi, mechi ambayo hata hivyo alifungwa na Nick Kyrgios wa Australia.

    Murray ambaye ni namba 159 kwa viwango vya ubora duniani kwa sasa ikiwa ni kutokana na kutocheza kwa muda mrefu aliwahi kuwa mchezaji namba moja duniani, na amewahi kushinda taji la Wimbledon mara mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako